Uwezeshaji wa Vijana wa Ulaya na Afrika

AEJK (Afrik-eŭropa junulara kapabligo, kwa kiswahili: Uwezeshaji wa Vijana wa Ulaya na Afrika) kwanza kabisa ni mkutano na kubadilishana kati ya vijana wazungumzaji wa kiesperanto kutoka Ulaya na Afrika. Katika mikutano minne (nchini Benin, Italia, Togo na Poland) pameandaliwa warsha kwa ajili ya kupata maarifa, mafunzo na kazi ya kikundi. Wakufunzi wataalam hushiriki katika mafunzo na matokeo yote (hati, ushauri/vidokezo, vifaa, na kadhalika) ya mikutano hiyo inapatikana kwenye tovuti yetu na kwa programu ya Android ambayo imeandaliwa katika mradi huo. Shukrani kwa Kiesperanto, lugha ya kijamii ya washiriki, TEJO inatoa mradi huu kuhusu elimu isiyo rasmi. Rasilimali zinapatikana kwa uhuru, kwa hio usisite kuzitumia kwa miradi yako.

Matokeo ya mradi

Washiriki wa mradi AEJK walijifunza jinsi ya kuwa wakufunzi, na kwa namna hio walipashwa wenyewe kuandaa mafundisho. Baada ya mafundisho waliandika muhtasari wa mafundisho. Muhtasari huo hupatikana hapa.

Maoni ya washiriki

Tuliuliza watu wachache walioshiriki kwenye mikutano maoni kuhusu mradi huu. Haya ndio majibu yao.

Kwa nini umeamua kushiriki katika mradi wa AEJK?

Mambo mawili tu muhimu yamenipendeza, kwa sababu hiyo nimeamua kushiriki katika mradi huu. Jambo la kwanza ni “kuwawezesha” vijana, na inalenga kufundisha na kuwafanya vijana hawa wakufunzi bora. Na pili ni ushirikiano wa mabara kuu mawili, ni kuhusu vijana wa Afrika na Ulaya; hio imenipendeza sana, kwa sababu ni nafasi nzuri kwa sisi wote kusikiliza habari kuhusu utamaduni wa wengine.
Cyprien (Benin)

Ni Kumbukumbu zipi unazo kuhusu mkutano wako na washiriki wengine wa AEJK?

Nakumbuka watu wazuri wenye manufaa. Walikuwa kutoka kwa tamaduni nyingine lakini hii haijalishi kwa sababu walikuwa na hamu kubwa ya kujua zaidi na walikuwa wazi. Nilifanya kazi nzuri nao wakati wa mafunzo. Nilihisi kama tulikuwa timu halisi.
Iwona (Poland)

Nilipenda sana ushirikiano na wakufunzi wengine wanne, tumefanya kazi pamoja kwa ufanisi na kwa shauku. Nilivutiwa pia na ubora na mapenzi ya kazi ya washiriki, wote walishiriki kwa makini, walitowa mafundisho bora na walijifunza mengi katika wiki.
Rogier (Uholanzi)

Je, una nia ya kutumia maarifa uliyopata katika mradi huu ? Ikiwa ndivyo, katika mazingira mapi ?

Ndiyo, nina nia ya kuyatumia katika mahali ya Kiesperanto ili kusaidia watu ambao wanataka kuboresha chama kama mimi, na nje ili kueneza maarifa kupitia njia inayofaa. Nitafanya hivyo katika miradi ya kijamii lakini pia kitaaluma.
Carlos (Uhispania)

Nina nia kabisa ya kutumia maarifa niliyopata katika mradi huu.
Mireille (Benin)

Picha: Łukasz Żebrowski

Partners

[tc-logo-slider logo_cat=”aejk”]